Friday, October 30, 2009

Mauaji ya Albino yanatokana na Asili.

Robinson Wangaso akiwa katika mafunzo ya internet

Pamoja na kupewa umuhimu na msukumo wa kisiasa mkubwa katika kushughulikiwa suala la mauaji ya Malbino nchini, mauaji hayo ni vigumu kukomeshwa kwa njia zinazotumika sasa kutokana na msingi kuwa yanatokana na jadi/asili ya watanzania na imani yao juu ya jamii hiyo.

Mauaji hayo ambayo yamekuwa yakiripotiwa kwa kiasi kikubwa katika kanda ya Ziwa mikoa ya Shinyanga, Mara, Kagera na Mwanza hususani wilaya za Geita, Magu, Misungwi, Sengerema na Kwimba.

Mikoa na wilaya hizo ambazo mauaji yamekithiri wengi wa wakazi wake wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa elimu ambalo limesababisha wao kujihusisha na vitendo vya kishirikina, ambapo wamekuwa wakienda kwa waganga wa jadi na kupigiwa ramli chonganishi.

Vitendo vya mauaji ya albino pia vimechangiwa na baadhi ya watu wanaojihusisha na shughuli za uvuvi na uchimbaji wa madini, ambapo wamekuwa wakiamini kuwa mvuvi akiingia na kiungo kimojawapo cha albino mfano nywele, damu, mfupa na ngozi kwenye mtumbwi wake hupata samaki wengi, hali kadhalika kwa mchimba madini.

Kufuatia imani hizo watu hao kwa asilimia ndio wanaochangia mauaji hayo kutokana na kutafuta vioungo hivyo kwa ajili ya shughuli zao hizo.

Lakini pia ongezeko la waganga wa jadi kwa asilimia kubwa nalo limechangia mauji ya albino, kutokana na kuwaagiza wafanyabiashara, wachimba madini na hata wavuvi baadhi ya viungo vya aklbino ili waweze kufanikiwa katika shughuli zao na hatimaye kuwa matajiri.

Mwenyekiti wa chama cha albino Mkoa wa Mwanza Bw. Alfed Kapole amesema kufuatia kuibuka kwa wimbi la mauiji yanayowalenga, hivi sasa wamekuwa wakiishi maisha magumu ya kujificha na hivyo kushindwa kufanya kazi za kujipatia kipato, sanjari na watoto kushindwa kwenda shule kwa kuhofia kuuawa.

“ Hata tunapokwenda hosptali au kwenye vituo vya afya baadhi ya wauguzi wamekuwa wakitunyanyapaa, yaani hawataki kabisa kugusana na sisi hivyo kushindwa kutoa tiba sahihi kwa mgonjwa, kwa ujumla hatuna sehemu ambayo tunaweza kupata msaada, kwani hata kwenye jamii inayotuzunguka kila wanapomwona albino wamekuwa wakishangilia kwa kumwita “DILI” sijui tukaishi wapi maana tumekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yetu” alisema Kapole.

Kutokana na mauji hayo hadi sasa takribani zaidi ya albino 44 wameuwa, ambapo ni kesi moja tu ndiyo imetolewa hukumu na watu watatu kuhumiwa kunyongwa hadi kufa mkoa Shinyanga.

kutokana na serikali kuona umuhimu wa kushughulikia tatizo hilo, waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alitoam uamuzi wa kufuta vibali vya waganga wote wa Tiba za jadi nchini ikiwa kama mkakati mojawapo wa kupambana na mauaji hayo.

Licha ya kufutwa kwa Leseni hizo, imani kuwa viuongo vya Albino vinaleta utajili itakuwa imefutwa katika akili za jamii hiyo na na itasaidia kuleta uelewa miongoni mwa wachimbaji madini, wavuvi na wafanyabiashara kuwa albino ni ulemavu kama ulivyo ulemavu mwingine?.Mfano wa Jamii kwanza na maggid Mjigwa ni mfano mzuri wa uwazi na uwajibikaji

watanzania tumekuwa wepesi kukimbilia kuiga mambo ya kigeni na kuacha mila zetu, kwa kufuata hata mambomyasiyofa, hili la mauaji kwa nini tusielewe kuwa Imani hizo zimepitwa na wakati na tumebaki kulingángánia.

Nimeweza kuongea na wazee wengi kutoka kanda ya ziwa ambao wanasema zamani Albino alionekana kama mkosi katika jamii na mazishi yake yalifanyika kwa siri pasipo watu kujua amabop siyo ndugu ama marafiki wa karibu, na baadhi yao walithubutu hata kuwanyoga watoto wadogo wakati walipozaliwa na endapo mkunga alibaini kuwa mtoto huyo alikuwa na ulemavu wa aina hiyo. Wizara ya afya tanzania

1 comment:

  1. mauaji hayo pia yanatokana na tamaa ya mali inayotokana na watu wenye upeo hafifu kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha ya biashara

    ReplyDelete