Tuesday, January 26, 2010

CHANGAMOTO KAZINI ZINATUKOMAZA, TUSIHOFU.

Kumekuwepo na badhi ya watumishi kupenda kuwasingizia watumishi wenzao makazini kwa mambo yasiyokuwa na msingi kwa malengo wa kuwakosanisha watu, marafiki, wafanyakazi ama mtu na mkuu wake wa kazi.

Kwa wale wanaowafanya vitendo hivyo wakumbuke kuwa nao ipo siku nao watafanyiwa vivyo hivyo japo katika maeneo tofauti ya kazi kutokana na usemi usemao, kila mtu atapimiwa kipimo kilekile alichopimia wenzake, na pia malipo ya mambo yote ya duniani ni hapa duniani. Katika mandiko matakatifu yanasema usihukumu ili nawe usije ukahukumiwa.

Inatia faraja kwa wanaofanyiwa hivyo wasife moyo kwani zamu yao imekwisha wangojewe thawabu kwa mambo hayo na wasikate tamaa bali wawe na moyo wa ujasiri na uvumilivu katika kuzikabiri changamoto hizo. Kwa hili namkumbuka hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere ambae aliwahi kusema ' Mtu Madhubuti mwenye moyo thabiti, haogopi matatizo bali hukomazwa nayo' mwisho wa kumnukuu.

Robinson Wangaso- Musoma MARA

Monday, January 25, 2010

WANAHABARI TUITUMIKIE JAMII BILA UBAGUZI - MARA

Waandishi wa habari katika mkoa wa Mara ipo haja ya kuamka na kuitumikia jamii kamayalivyo malengo na madhumuni ya wanahabari ambayo ni kuelimisha, kuhabarisha kutahadhalisha kuburudisha pale inapobidi.

Yapo matukio mengi ambayo yamekuwa hayaripotiwi japo taarifa ya matukio hayo kuwafikia wanahabari na baadhi yetu kuyapuuza kwa sasababu mbalimbali zikiwemo za kutolipwa gharama za utumaji wa habari hizo japo baadhi ya matukio hayo ni ya mauaji na hata kunyanyaswa kwa watu wa hali ya chini kimaisha. Nadhani sisi wanahabari ndiyo kimbilio la wasiyo na pa kukimbilia.

Umefika wakati wa kujirekebisha na kubadirika ili tuitumikie jamii, ni dhahiri hakuna atakaebisha juu ya weana

Friday, January 22, 2010

UMUHIMU WA USHIRIKIANO (Jessie )

Nimeamini kuwa upo umuhimu mkubwa katika kushirikiana na watu mbalimbali na kuachana na dhana ya kuwa na ubinfasi.

Nimeweza kujifunza mambo mengi kwa kushirikiana na watu mbali mbali Jessie Boylan mwandishi wa habari wa shirika la kimataifa mwenye umri mdogo lakini aliye makini na kazi yake.

Robinson Wangaso

Thursday, January 21, 2010

RAFIKI YANGU SIKUMFAHAMU ANA WIVU

Ni vigumu kufahamu tabia ya kila mmoja licha ya kuishi na mtu kwa muda mrefu hususani marafiki ambao tunao karibu.

Imewahi kunitokea kushauriwa vibaya na rafiki yangu kuacha kufanya mambo yenye mafanikio kwa kuwonawivu. Je wewe mkasa kama huu umewahi kukutokea?

Robinson Wangaso

MAPENZI / NGONO KAZINI !!! IWEPO SHERIA??

Sote tunatambua neno mapenzi linaashilia uhusiano mwema, japo Neno hilohilo kwa matumizi ya sasa na hali halisi limeweza kusababisha mtafaruku mkubwa kati ya mtu na mtu na hata kati ya wanandoa na kusababisha mahusiano ya watu hao kuwa mabaya, haya siyo mapenzi kama neno linavyojieleza kwani hakuna upendo hata kidogo, bali ni NGONO maofisini ambayo inatumoka kuzorotesha ufanisi wa kazi katika maeneo hayo.

Kwa leo tuangali mapenzi katika maeneo ya kazi hasa zaidi nazungumzia kati ya wakuu wa vitengo (Maofisa) ambao hupenda kuitwa mabosi jina baya kabisa na lisilofaa kwa Mtanzania mwenye nafasi ya kutumikia watu kujiita/ kuitwa ''BOSS''

Ni dhahili tunatambua mapenzi yanaweza kuvuruga ufanisi na utendaji kazi na hata kuondoa heshima dhidi ya wasaidizi, mapenzi katika ofisi nyingi yamesababisha watendaji wengi kuacha kazi kutokana na fitina na chuki dhidi ya wakubwa wao wa kazi. Pia wakubwa hao wanapolewa mapenzi huweza kuwapatia waangalizi wa ofisi yao (ps)madaraka yasioendana na sifa na uwezo wao.

hali kana hii inatupeleka wapi jamani?? nanyi semeni kamani haki kuona wazee wanatembea kimwili na watoto wadogo kwa kuwadanganyishia posho, malupulupu pamoja na nafasi ambazo siyo halali.

Kwa upande wa hao mabinti wadogo ambao wanalazimika kuwa na uhusiano wa kimapenzi ha hao wanaojiita MABOSS, ni kweli pamoja na kupewa upendeleo huo unadhani wako salama?? Ikitokea huyo mtu kahamishwa au kafariki kwa vile alikuwa anategemea kubebwa unadhaninutendaji kazi wake utakuwa vipi.

Kutokana na hali hiyo ya kubebwa kama JENEZA hivi ni kweli mfanyakazi huyo atakua salama na kazi yake kwa kutembea na Boss wake au kesho akipata mwingine anaempendeza machoni zaidi kuliko yeye mabo yatakuwa vipi??!! naombeni kwa hili nalo mnishauri.

mbaya zaidi hawa wanaojiita wafanyakazi wenye mahusiano ya kimapenzi wa Maboss wamekuwa wakitumia uhusiano huo kuwavuruga watumishi wenzao kwa wakubwa wao wa kazi na kutokana na wakubwa kulewa mapenzi huwachukia wafanyakazi hao bila kufanya uchunguzi wa kina.

Hawa wazee nao pia tuwape somo, wasiburuzwe na vibinti kisa wanamahusiano ya kimapenzi. wakumbuke kupewa nafasi yoyote ile ni kwa ajili ya kutumikia watu na siyo kujipatia vijitoto tena ni sawa na kuvibaka vitoto / vibinti hivyo ambavyo vinachafuliwa damu buila kujijua.

Baadhi ya mabinti hushiriki mapenzi na wazee hao kwa kuhofia kupoteza kazi au kupata upendeleo maalumu lakini wakati huo huo huwa na wapenzi wao vijana hata katika iofisi hizo ambao ni rika moja, hali hiyo inapojulikana maboss hao huwachukia wanaotembea na wasaidizi hao bila kujua siyo haki wala sawa kwa mzee kama huyo badala ya kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa wafanyakazi wake, anakuwa ndie mwanzilishi wa ugomvi, fitina kutoka na kuchangia binti mdogo kimapenzi na vijana.
Hapa naona umuhimu wa kutungwa kwa sheria ya mapenzi kazini kwani ukiongea na mabinti wengi wanaotembea na wakubwa wao wa kazi watasema walibakwa, walitishiwa kupoteza kazi, walipewa nafasi ya upendeleo na hata madaraka yasiyowasitahili hadi kushawishika.

Haya nanyi semeni.

Robinson Wangaso nahitaji ushauri na maoni yako.

USHIRIKINA KAZINI / MAOFISINI JAMANI

Ni kweli kwa siku za hivi karibuni, kumekuwepo na malalamiko mengi dhidhi ya vitendo vya kikatili na kinyama dhidi ya mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino)kutokana na vifO vyenye simanzi na masikitiko makubwa DHIDI YA BUNADAMU WENZETU.

Hali hii inatokana na wasomi tulionao kuwa na imani potofu juu ya ushirikina. Kama Mtu aliyesoma na kufuzu shahada/ stashahada, bado anaamini juu ya ushirikina. Mtu kama huyo kabla ya kuanza kazi anaanzia kwa mganga wa JADI ndipo aanze kazi. Wengine huenda mbali zaidi na hata kudriki kupeleka katika ofisui wanazofanyia kazi waganga ili wazindiki ofisi hizo wakidhani pasipo kufanya hivyo hawatakuwa salama. Je, hivi tunao wasomi au ni vyema turudi kwa Mababi na Mabibi zetu tuwaachie ofisi waziendeshe? kwani pamoja na kusomabado tunaamini bila ushirikina mambohayaendi.

Kama msomi anaamini ushirikina, anaenda kwa mganga kabla ya kuanza kazi au akazindike ofisi, Unadhani kati ya mganga na Mtu huyo anaejiita Msomi nani aachiwe ofisi. Nasisitiza hili kwa sababu huwezi kujua kesho mganga atamshauri nini huyo mwajiriwa mwenye kutegemea mganga na pasipo Ushirikina hajiiaminin kuwa yupo kazini.

Naombeni ushauri na mawazo yenu juu ya suala hili. Hawa wasomi Tegemezi, hawatufai kamwe kuendelea kuwa nao katika ofisi yoyote ile ni kuwa na mtu hatari kwa maendeleo ya taifa. Ni msimamo na Mtazamo wangu tu, Nawe toa wako.

Robinson Wangaso