Sunday, September 19, 2010

WATANZANI WATIA FORA SWEDEN


na Robinson Wangaso


Na Robinson Wangaso

Waliwavuta vijana hao wa Kiswedishi hasa katika mihadhara mbalimbali ya kubadilisha mawazo na uzoefu.

WATANZANI WATIA FORA SWEDEN



waliweza kuwafurahisha vijana wenzao wa kisweden ambao pia wako katika harakati za kuja nchi Tanzania kujifunza mazingira, Tamaduni, usawa wa kijinsia na Democrasia.



Ni vijana 14 wa kitanzania

SIKU TISINI ZA MASOMONI SWEDEN.

Na Robinson Wangaso - Sweden





Hakika kutembea ni kujifunza, pampja na kuwa nilikuwa nchi Swedeni kwa ajili ya masomo lakini kuna elimu kubwa niliyoipata nje ya darasani kwa kujifunza mambo mengi yakiwemo utunzaji wa mazingira, jinsi watu wanavyojichukulia au kujiheshimu na kutojiheshimu kwa nkuwa wapo ulaya.

Kwangu kwenda ulaya siyo jambo muhimu, muhimu ni matokeo baada ya kutoka Ulaya nini nitajifunza na ni namna gani nitaweza kubadilisha hali fulani katika maisha na namna ya kusaidia jamii ya Watanzania.

Wapo walioenda mbali zaidi na hata kutaka kukana desturi zao wakidhani ulaya ndiyo mambo yote, lakini nilichokibaini ni kuwa WAZUNGU wanayo hamu kubwa ya kujifunza kutoka kila kona hata kwa WAAFRIKA ambao tumekuwa kujijidharau kila siku.

Haba baadhi ya Watanzania wakiwa nchini Sweden

Wednesday, September 15, 2010

KIKWETE UNAKUMBUKA AHADI YAKO MARA

Na Robinson Wangaso, Musoma. 0765632944/ 0712735318

Imebaki miezi mitano tu, na siyo miaka mitano ufanyike uchaguzi mkuu bila kutekelezwa kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa kwa wakazi wa mkoa wa Mara ya kukamilisha ujenzi wa hospitali ya mkoa wa Mara lililopo katika eneo la Kwangwa manispaa ya Musoma kama alivyosema kwa miaka mitano Hospitali ya mkoa itakuwa imekamilika.


Akihutubia umati mkubwa katika mkutano hadhara wa kampeini mwezi Oktoba 2005 uliyohudhuriwa na wananchi wa mkoa huu kutoka wilaya zote rais Kikwete akiwa mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM aliahidi kuwa mkoa hauna hospitali yenye hadhi kutokana na uliyopo kuwa na majengo chakavu na haitoshi kutokana na ongezeko la wagonjwa kwani majengo ya hospitali hiyo yalijengwa zama za mkoloni.

" Mkoa wa Mara hauna hospitali yenye hadhi ya kimkoa, hii iliyopo imepitwa na wakati. Ni ahadi yangu kwenu kwa kipindi cha miaka mitano Hospitali yenu mpya itakuwa inafanya kazi, hii ni ahadi yangu kwenu na kamwe hamtanisuta baada ya miaka mitano" alisema raisi Kikwete.

Miaka ya 1980 wananchi wa mkoa wa Mara wakiwemo wakulima ambao walikuwa wakikatwa shilingi tatu kwa kila kilo moja ya pamba ambayo ilikuwa ikiuzwa katika vyama vya ushirika kwa wakati huo walichangia kwa zaidi ya miaka mitano ujenzi wa hospitali mpya ya mkoa ambapo jengo lake halikukamilika na kuishi njiani kwa kile kinachodaiwa kuwa usimamizi na matumizi ya fedha hizo haukuwa mzuri.

Ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo ilifikia ghorofa Tatu na kuishi hapo umekuwa ni kero kubwa ya wakazi wa mkoa wa Mara kwa serikali ambayo ilishindwa kusimamia fedha hizo za wananchi na kuwachukulia hatua wale waliokuwa wamekabidhiwa dhamana ya kusimamia ujenzi kwa niaba ya wananchi ambapo jasho la wanyonge kupotea bure bila huruma.

Kutokana na hali hiyo kuonyesha wananchi kupunguza imani na serikali yao kwa kushindwa kutimiza na kukamilisha azma ya wananchi, viongozi mbalimbali wakiwemi wale wanaowania nafasi mbalimbali za kisiasa wakiwemo wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM wamekuwa wakitumia kero hilo katika kampeni wakitoa ahadi ya kukamilisha ujenzi huo pindi wakichaguliwa kwa kuisukuma serikali na baada ya kuchaguliwa huishia mitini.

Kero hiyo pia alifikishiwa rais Kikwete na alichaguliwa kuwa rais aliporudi katika ziara yake ya Kwanza mkoani Mara mwezi Januari 2006 ya kushukuru wakazi wa mkoa wa Mara na wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani hapa Augosti 9 hadi 14 2006 alisema Serikali imekubaliana Kanisa Katholiki kukamilisha ujenzi huo ambao gharama za ujenzi zitatolewa kwa ushirikiano baina ya serikali na Kanisa hilo huku usimamizi wa ujenzi utakuwa chini ya kanisa.

Katika hotuba hiyo ambayo aliitoa katika viwanja hivyo hivyo vya shule ya msingi Mukendo, rais alisema hospitali hiyo itakalimishwa ujenzi wake na kufunguliwa kama hospitali ya Rufaa ili kusongeza karibu huduma ya matibabu kwa wananchi wa mkoa wa Mara na mikoa mingine ya kanda ya ziwa ambayo hawana hoaspitali za Rufaa na kuahidi kupanuliwa iliyokuwa hospitali ya mkoa ya zamani.

Wananchi wameshuhudia upanuzi ukifanyika lakini bado wanahoji, nguvu zao na michango yao ambayo waliielekeza katika ujenzi wa hospitali ya Kwangwa na kuahidiwa na viongozi wa kisiasa wakiwemo wale wa kitaifa kuwa ingekamilika zimetupwa au tena katika chaguzi zijazo ahadi zitaendelea kutolewa ambapo ni zaidi ya miaka 20 jengo hilo ambalo inasadikika limejengwa kwa ustadi mkubwa bila kukamilika.

Akionekana ni mwenye Ari, Nguvu na Kasi ya kutekeleza ahadi hiyo, rais alirudi Musoma Mwezi Agosti 31 mwaka 2006 kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa askofu wa jimbo la Musoma Mhashamu Justin Tetemu Samba ambapo alirudia kauli yake mbele ya waamini wa kanisa hilo na wananchi walijitokeza katika mazishi hayo kuwa mazungumzo na makubaliano baina yake na Askafu yalikuwa yamekamilika na hivyo aliomba msimamizi wa jimbo atakaechaguliwa na kanisa aendeleze juhudi hizo bila kuchelewesha ili serikali itoe fedha na ujenzi huo uanze.

" Mkoa wa Mara umepoteza mtu muhimu sana katika huduma za kiroho na maendeleo ya kijamii, Serikali ilikuwa na mkakati wa kushirikiana nae katika ujenzi wa Hospitali ya Rufaa mkoani hapa" alisema Rais Kikwete wakati wa salamu zake wakati wa mazishi hayo.

Mwezi Agosti 27 hadi Sepemba 1 2007 waziri mkuu wa wakati huo Edward Lowassa ambae alifanya ziara ya kikazi mkoani Mara ambae alionyesha kwa kipindi cha uongozi wake kufuatilia masuala muhimu za mkoa wa Mara yakiwemo mapigano ya koo za kabila la wakurya Tarime alifanya ziara mkoani Mara na kutembelea jengo hilo la Hospitali ikiwa ni kutaka kutekeleza ahadi ya seriakali ambapo alielezwa na msimamizi wa jimbo wa wakati huo Padre Julius Ogola kuwa kanisa lipo katika mchakato wa kuanza ujenzi tatizo ni fedha kwani ujenzi huo unagharimu fedha nyingi na serikali isaidie isaidie upatikanaji wake ili kazi ianze na waziri mkuu huyo aliahidi kuchukua hatua kwa haraka kwa ahadi hiyo ya serikali ya awamu ya nne kwa wananchi wa mkoa wa Mara.

Lowassa kaondoka madarakani, lakini najua waziri mkuu yupo na ofisi ya rais bado ipo? Je ni ninakila sababu ya kujihoji tatizo lipo wapi? serikali imesahaua ahadi zake au imedhamilia rais ili akutwe na wananchi wa mkoa wa Mara ambao ni wa wazi na wakweli wasio na soni hata kidogo baada ya miaka mitano ya serikali ya awamu ya nne kumalizika.

Wakati wa askofu mpya wa kanisa hilo Mhashamu askofu Michael Msongazila ulioyofanyika katika kanisa kuu la Maria mama wa Mungu, Lowassa alihudhuria sherehe hizo na kumshika mkono Mara baada ya kusimikwa rasmi na kumhakikishi kuwa serikali itashirikiana naye katika ujenzi wa hospitali ya rufaa. Lowassa aliondoka na serikali?


Hivi ni kweli ahadi hiyo haina kumbukumbu au kuondoka kwa Lowassa hakuna tena kiongozi wa serikali tofauti na rais kufuatilia ahadi alizotoa rais wakati wa kampeni ili zitekelezwe. Tunajua kuwa rais anazo shughuli na majukumu mengi, ndiyo maana wapo mawaziri, wakuu wa mikoa na ha wilaya ili kumsaidia kazi kutokana ma mfumo na mgawanyo wa madaraka ikiwa ni pamoja na kumkumbusha katika maeneo yao nini kinaendelea.

Kama ndiyo kwani ahadi siyo jambo muhimu kwa mkuu wa mkoa kumkumbusha rais, au tunasubiri kumpatia taarifa za matukio ya mauaji na mambo mengine huku ahadi hizo zikiwa zinakumbukwa vizuri na wananchi na wanasubiri wakati wa kampeni wamuulize "mzee ilituahaidi, ulisema kamwe hatutakuja kukusuta" ? Je rais utajibu vipi hapo?

Natumaini majukumu muhimu ya viongozi serikali katika mikoa ni pamoja na kujua wananchi wan shida gani na kipi wanamdai kiongozi wao wa kitaifa ndiyo maana ya uwakilishi na siyo kueleza mazuri tu kuwa unakubgalika mzee, je kwa nini msimwambie kuwa wananchi wanamdai nini ili watimizie.

Rais aliona umuhimu huo wa kuwa na hospitali ya mkoa ambao ni dhahili kila mmoja wetu anaukubali kutokana na huduma ya afya katika mkoa wa Mara kuwa inahitaji kupewa msukumo wa pekee kutokana na mkoa wenye wilaya sita unayo hospitali moja tu ya wilaya katika wilaya ya Tarime, huku wilaya ya Bunda wakitumia hospitali teule DDH inayomilikiwa na kanisa la KKKT, Wilaya ya Serengeti na Rorya hospitali zilizopo zinamilikiwa na kanisa la Menonite, Musoma vijijini na mjini hakuna hospitali ya wilaya na zinategemea hospitali ya mkoa.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

BUTIAMA WAMPONGEZA JK

Na Robinson Wangaso, Musoma - MARA 0784301526, 0765632944

Wananchi wa kata za Butiama ,Masaba, Muryaza na Butuguri wilayani Musoma vijijini mkoani Mara wamefanya maandamano ya kumpongeza rais Jakaya Kikwete kwa kuiteua Butiama kuwa wilaya mpya.

Sherehe hizo zimefanyika jana kijijini Butiama katika ukumbi wa Joseph Kizurira Nyerere ambao ulishatumika kuikutanisha Halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM chini ya uongozi wa mwenyekiti wa chama hicho taifa Jakaya Kikwete na kutoa pendekezo la jina la Butiama kupewa wilaya mpya itakayoundwa kutoka wilaya ya Musoma vijijini.

Maandamano hayo ambayo yameanzia katika vijiji mbalimbali vya kata hizo yamepokelewa mkuu wa wilaya ya Musoma ambae aliwakilishwa na Afisa Tarafa ya Makongoro Lucy Makenge na viongozi mbalimbali waandamizi kutoka halmashauri ya wilaya.

Bi Lucy Aliwaasa wakazi wa Butiama kuwa tayari kushirikiana na kuijenga wilaya hiyo mpya ili kumuenzi Baba wa Taifa Mwali Julius Kambarage Nyerere kwa mambo mazuri aliyoyafanya katika kuongoza nchi na amewathibitishia wananchi hao kuwa saerikali ya jamuhuri ya Muungano itatimiza azma yake ya kuanzishwa na kuiendeleza wilaya mpya ya Butiama.

" Kwa niaba ya familia ya mwalimu Nyerere, anatoa shukrani kwa Rais Kikwete kwa kuona umuhimu wa kuanzisha wilaya mpya yenye jina la Butiama, kijiji alichozaliwa Baba wa Taifa" alisema Lucy, Afisa tarafa.

Akiongea kwa niaba ya wazee wa kijiji cha Butiama, Mzee Jackton Nyerere alisema " Nyerere Burito baba yake na mwalimu Nyerere kabla ya kifo chake aliwahi kutabiri kuwa Butiama itakuwa na wageni wa kila aina, kuanzishwa kwa wilaya hii ni kukamikilika kw utabiri wa Chiefu huyo wa kabila la wazanaki" alisema mzee Jackton Nyerere.

Nae Mwalimu Jack Nyamwaga alisema kikao cha Halmashauri kuu ya taifa kufanyika Butiama kilikuwa na jambo ambapo Tanzania imeweza kuazimia mabo mengi ikiwemo azimio la Arusha, siasa na kilio, Azimio la Musoma anazimio la Mwisho kwa mjibu wa mwlimu huyo ni kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Butiama.

Hafla hizo pia zimeandaman na ngoma, kwaya, michezo mbalimbali ziikiwemo ya asili kutoka kabila la Wazanaki, Waikizu ambapo maelfu ya wananchi kutoka kata jirani na Butiama wamehudhuria.

kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Butiama Zakaria Wambura alisema Ris Kikwete amemuenzi baba wa taifa kwa vitendo kwa ambapo wilaya hiyo mpya itakuwa chachu katika kuinua hali za maisha ya wananchi wa kata hiyo na kata jirani

Wakati huo huo mmoja wa wanafamilai ya mwalimu Veronica Jackton Nyerere ametangania nia ya kuwania nafasi ya ubunge vitri maalumu mkoani Mara kupitia ambae amewataka wananchi hao kutoshangilia wilaya mpya na kuwapisha wageni, bali wafanye kazi kwa bidii.

"Wanabutiama tuwe wabunifu ili wilaya iwe wilaya mfano ya kumuenzi baba wa taifa na tukubali kubadilika na kuwasomesha watoto ili kuendana na soko la ajira" alisema Veronica Nyerere mbele ya umati huo.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,

UCHAGUZI SWEDEN

Na Robinson Wangaso, Sweden +46722071257.

Jumapili ijayo ni siku muhimu kwa Wananachi wa Sweden ikiwa ni siku ya uchaguzi wa kuwapata viongozi wao wa kisiasa katika ngazi ya majimbo, mkoa na wawakilishi katika Bunge sawa na ngazi ya kitaifa.

lakini kwa Waswidi zoezi la kupiga kura limeanza wiki moja kabla kwa wale anaodhani siku hiyo hawatakua na nafasi kwenda kupiga kura wanafika kwa wakati wao wanaopenda katika vituo vilivyopo wanapiga kuza zao na kuondoka.

Kilichonistajabisha zaidi ni pale nilipotembelea kituo kimojawapo cha kupiga kura katikati ya jiji la Stockholm ambao ndiyo mji mkuu wa nchi hii na kujionea jinsi kura hizo zinavyopigwa katika hali ya uwazi.

Japo kura ni siri lakini wakati mtu anapopiga kura yake katika eneo la kupigia kura unaweza kusogea karibu bila wasiwasi kama ilivyozoeleka nyumbani nchini Tanzania bila shaka nawe utapiga kura yako na kuondoka.

Zaidi ya hapo katika chumba cha kupigia kura nilikuta watu wawili ambao ndio wasimamizi wa upigaji kura hakuna mawakala wa vyama vya siasa na watu wanawaamini na kupiga kura zao bila kuhofia kuwa kura zitaibiwa jambo ambalo lilinishabgaza kuona hivyo tume ya uchaguzi kusimamia upigaji kura kwa kuaminiwa na wananchi pamoja na wanaogombea kupitia vyama mbalimbali vya siasa.

Kuhusu kampeni kama tunavyojua juma la mwisho huwa ni vurugu mechi lakini ukiwa nchini Sweden hutajua kua ni wiki ya Uchaguzi kama hujaambia na mtu kwani kampeni hazifanyiki katika mikutano ya hadhara bali ni kupitia vyombo vya habari na kuwasambazia majumbani vipeperushi wananchi kupitia masanduku yao ya Barua (Posta)vinavyoelezea sera za vyama vyao.

Pia katika baadhi ya niji na majiji unakuta wafuasi wachache wa vyama fulani wakigawa machapisho hayo ya sera kwa watu wanaopenda kujua juu ya chama hicho lakini kazi hiyo inafanyika katika hali ya utulivu na hakuna vurugu wala kulazimishwa kuchukua kipeperushi bali kwa kuombwa kwa lungha ya unyenyekevu kuchukua vipeperushi.

Mfumo wa uchaguzi ni kuchagua Chama na siyo mtu, kila chama kinakua na orodha ya wagombea ambao watateuliwa kuingia bungeni Mara baada ya uchaguzi ikiwa kitashinda lakini watakaoteuliwa inategemeana na asilimia ya ushindi au kura chama kilichopata.

Lakini pia mpiga kura kabla ya kupiga ataangalia orodha ya wagombea wa chama anachokipenda na ikia ataona mtu anaempenda amewekwa katika orodha nafasi ya mwisho kwa umuhimu anaweza kuzungushia jina lake kuonyesha kua mtu huyo anapenda apewe nafasi kutokana na kua anapenda aiingie Bungeni.


Pamoja na wagombea kupewa nafasi za kipaumbele na vyama vyao pia wananchi au wapiga kura wanayo fursa ya kubadilisha orodha kwa kumpigia mtu furani aliyopewa nafasi ya mwisho na kupewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwawakilisha katika bunge ikia ni namna ya kuthamini na kuheshimu wanachokipenda wapiga kura.

Zaidi ya vyama Saba zinashiriki katika uchaguzi utakaofanyika Wiki hii hapa nchini Sweden huku hakuna kelele wala vurugu zozote zinazoashiria kuwepo na uchaguzi watu wakiendelea na shughuli zao kamakawaida.

Wanaoruhusiwa kupiga kura ni raia wa Swedena na wageni ambao siyo raia lakini wenye vibali (VISA) za zaidi ya miaka mitatu kuishi nchini humo nao wanayo haki ya kupiga kura hata kama siyo raia wa nchi hiyo.

Sweden ni nchi inayofuata mfumo wa utawala wa Kifalme lakini ikiwa na vyama vingi vya siasa na kiongozi mkuu na msimamizi shughuli za serikali ni waziri mkuu ambae huchaguliwa kwa kupigia kura kila baada ya miaka minne.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,

Thursday, June 10, 2010

MAUAJI YA WANYONGE MARA HAYAPEWI KIPAUMBELE

KUMEKUWA NA MAUAJI ya mara kwa mara Yaliyotokea katika mkoa wa Mara na mengi ya mauaji hayo kutoripotiwa kabisa katika vyombovya habari pengine ni kutokana na waandishi wa habari kutoona umuhimu ama kutofuatiliamatukio hayo sambamba na viongozi kupuuza wakiwemo makamanda wa jeshilapolisi wa kanda maalum Tarime /Rorya na mkoa wa Mara.

Kabla ya kuwanyooshea vidole viongozi hao hebu kwanza nianze na sisi wenyewe kama waandishi wa habari ambaotumekuwa tukisikia matukio ya watu kuuawa na kutofuatilia huku tukifuatilia habari za vikao na mabaraza ya madiwani na kikutano ya wabunge kwa kuwatunajua kuna posho huko.


Hivi mtu kuuawa haijalishi kipato chake, mtanzania mwenye haki na thani ya kuishi kamabinabamu anauawa usitake kuandika habari hiyo na badala yake siku hiyo unaandika habari ya mbunge ama diwani katoa ahadi ya kukarabati barabara ama kachangia ujenzi wa sekondari, kweli hiyo ndiyo dhamani tuliyonayokatika kuielimisha, kuihabarisha Jamii ya watanzania kamawana habari?

Kwa upande wa viongozi watawala na makamanda na jeshila polisi, Kuna badhi ya matukio yakitokea hujitahidi kutoa taarifa kwa waandishi hata kwa kuwatafuta kwasimu, lakini baadhi ya matukio yakiwemo mauaji wa watu wenye kipato kidogo ambao bndio watanzania halisi na walio wengi wenye mchango mkubwa katika taifa lao, wanaoiweka serikali madarakani kuupuuzwa na kutotolewa taarifa endapo hakuna mwandishi naliyefuatilia amakuuliza juu ya mauaji hayo pengine kwakutopata dokezojuu ya tukiohilo.

Viongozi na waandishi wa Habari hatuwatendei haki watanzania walio wengi.

Wednesday, March 24, 2010

VIONGOZI WETU

Umefika wakti wa kuambiza ukweli kwani kila mtu katika nafasi yake anao uwezo wa kufanya kama siyo kuchangia katika jamii yake. kuna viongozi wanaodhani kuwa wanamuenzi Baba wa taifa Mwalimu julius K. Nyerere kwa kuwa katika chama au kubakia katika itikadi fulani, hii siyo kweli na ni wenda wazimu. Sina budi kuwaambia adhanie amesimama angalie asianguke.

Mwalimu alisema " heshima ya mtu haitokani na mali yake, cheo au elimu bali utu wake" pia wapo viongozi wanaodhani kuwa baba wa taifa ni mali yao japo ukiangalia mambo wanayoyafanya ni tofauti kabisa.

Tuesday, March 9, 2010

Kuhamisha Wafugaji Tarime Siyo Suluhisho- Uharifu

Kwa mara nyingine narudia kusema, hakuna njia moja katika kutatua matatizo, lakini nakubaliana na kauli ya kuwa kukimbia matatizo siyo njia ya kuepuka matatizo, haya ni maneno ya wahenga ambao walinena.

Kauli ya mkuu wa mkoa wa Mara kanari Enoce Mfuru ya kusema kuwa wafugaji walio katika wialya ya |Tarime wahamishwe kama njia ya kupunguza vitendo vza wizi wa mifugo na mauaji nasema kamwe siyo njia wala suluhisho la matatizo ya Tarime.

Tarime imekuwa katika hali ya machafuko kutokana na kilimo cha Bangi, Uhasama wa kugombania ardhi na mipanga ya asili iliyowekwa na mkoloni, kulipiza kisasi dhidi ya uhasama wa siku nyingi na wizi wa mifugo unaofanywa na baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo.

Kilimo cha bangi kimechangia kwa kiwango kikubwa na kufanya wananchi wa wilaya ya Tarime wakiwemo vijana ambao kwa kiasi kikubwa wameathiriwa na uvutaji wa Bangi.

Kuwahamisha wananchi hao na kuwapeleka katika wilaya za Bunda, Musoma vijijini, na Serengeti haitawabadilisha tabia wala kuacha vitendo vya uharifu.

Kuhamisha wafugaji haina maana kuwa wafugaji ndiyo wezi bali serikali inapaswa kudhibiti wizi na vitendo vya uharifu na siyo kuhamisha wafugaji.

Kama wilaya ya Serengeti hali ya usalama na imewezekana kwa Tarime inashindikana VIPI???????.

Waziri mkuu aliyepita Edward Lowassa alikuwa na nia wa kweli katika kutatua matatizo ya Tarime kwa njia shirikishi ambapo wananchi walipewa fursa ya kutoa mchango wao juu ya kumaliza/ mgogoro huo hatua ambayo imetelekezwa na kutumia nguvu za dola kwa kuongoze maaskari ambao hawanakuleta mabadiliko yoyote.

LOWASSA KWA HILI UTAKUMBUKWA SANA NA WANATARIME.

Sunday, March 7, 2010

Mauaji Mara Serikali haijadhamilia kuyakomjesha.

Ni wahenga walisema ''usipoziba ufa utajenga ukuta, na udongo upasnde ugali maji, bila kusahau samaki mkuje angali mbichi.'' Metahli hizi zote zinamaana kubwa katika hali ya maisha ya wakazi wa mkoa wa Mara.

Kadharika wananuchumi wanasema hakuna njia sahihi ya kukuza au kuboresha uchumi isipokuwa njia yoyte ile itakayokuwa na mafanikia kwa wakati furani kutokana na hali halisi ya maisha na mweleke wa wakati huo.

Kumekuwa na mauaji ya mara kwa mara mkoani Mara huku serikali ikiwa imeweka askari polisi na kuunda kanda maalumu ya mkoa wa kipolisi Tarime / Rorya pasio mafanikio. Tena baada ya mkoa huo kuundwa matukio yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku.

Serikali inajua ukweli kuwa wananchi wa Tarime walisahaulika hadi kujiona kuwa hawapo Tanzania na kuanza kujifanya mabo wanavyotaka.

Pia kuweka askari bila kuangalia chanzo cha machafuko hayo siyo suluhisho wala ufumbuzi la tatizo hilo la wakazi wa Mara na mauaji yanaoendelea siku hadi siku.

Naamini serikali ikiwashirikisha wakaazi wa Mara kama walivyo wakweli na wawazi wenyewe watatoa ufumbuzi wa kukomesha hali hiyo tena bila gharama kubwa wala kuumiza wananchi kwa namna yoyote ile.

Serikali ikubali ushauri na itumie uongozi shirikishi, wananchi wahusike kutatua matatiyo yao wenyewe kama ilivyo adhina ya dhamira ya kuanzishwa kwa serikali za mitaa hapa nchini ya kurejesha madaraka mikononi mwa wananchi wenyewe. Sasa mbona mnayang'ang'ania hamtaki kuwaachia / kuwashirikisha wana - Mara katika kutafuta ufumbuyi.

Pia viongozi waongoze na wafuate mifano yab viongozi waliotangulia, Hapa siktasita Kumta Aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani ya nchi miaka ya 90 katika serikali ya awamu ya pili Augostino Ryatonga Mrema ambae aliweza kutuliza wilaya ya Serengeti Mkoani Mara ambayo ilikuwa tishio kubwa kwa usalama wa raia, mali zao na hata wageni tena ilikuwa hatari zaidi ya mara kumi ukilinganisha na Tarime inayohangaisha watu na kuharibu sifa ya Tanzania kwa kuhofia kuwa Mara ni hatari kiasi hicho. kwa wakati huo ambapo hadi sasa Serengeti ni swali.

Mrema bado yupo kwa nini asitumike.

MARA NI IMARA NA SIYO TISHIO.

Tuesday, January 26, 2010

CHANGAMOTO KAZINI ZINATUKOMAZA, TUSIHOFU.

Kumekuwepo na badhi ya watumishi kupenda kuwasingizia watumishi wenzao makazini kwa mambo yasiyokuwa na msingi kwa malengo wa kuwakosanisha watu, marafiki, wafanyakazi ama mtu na mkuu wake wa kazi.

Kwa wale wanaowafanya vitendo hivyo wakumbuke kuwa nao ipo siku nao watafanyiwa vivyo hivyo japo katika maeneo tofauti ya kazi kutokana na usemi usemao, kila mtu atapimiwa kipimo kilekile alichopimia wenzake, na pia malipo ya mambo yote ya duniani ni hapa duniani. Katika mandiko matakatifu yanasema usihukumu ili nawe usije ukahukumiwa.

Inatia faraja kwa wanaofanyiwa hivyo wasife moyo kwani zamu yao imekwisha wangojewe thawabu kwa mambo hayo na wasikate tamaa bali wawe na moyo wa ujasiri na uvumilivu katika kuzikabiri changamoto hizo. Kwa hili namkumbuka hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere ambae aliwahi kusema ' Mtu Madhubuti mwenye moyo thabiti, haogopi matatizo bali hukomazwa nayo' mwisho wa kumnukuu.

Robinson Wangaso- Musoma MARA

Monday, January 25, 2010

WANAHABARI TUITUMIKIE JAMII BILA UBAGUZI - MARA

Waandishi wa habari katika mkoa wa Mara ipo haja ya kuamka na kuitumikia jamii kamayalivyo malengo na madhumuni ya wanahabari ambayo ni kuelimisha, kuhabarisha kutahadhalisha kuburudisha pale inapobidi.

Yapo matukio mengi ambayo yamekuwa hayaripotiwi japo taarifa ya matukio hayo kuwafikia wanahabari na baadhi yetu kuyapuuza kwa sasababu mbalimbali zikiwemo za kutolipwa gharama za utumaji wa habari hizo japo baadhi ya matukio hayo ni ya mauaji na hata kunyanyaswa kwa watu wa hali ya chini kimaisha. Nadhani sisi wanahabari ndiyo kimbilio la wasiyo na pa kukimbilia.

Umefika wakati wa kujirekebisha na kubadirika ili tuitumikie jamii, ni dhahiri hakuna atakaebisha juu ya weana

Friday, January 22, 2010

UMUHIMU WA USHIRIKIANO (Jessie )

Nimeamini kuwa upo umuhimu mkubwa katika kushirikiana na watu mbalimbali na kuachana na dhana ya kuwa na ubinfasi.

Nimeweza kujifunza mambo mengi kwa kushirikiana na watu mbali mbali Jessie Boylan mwandishi wa habari wa shirika la kimataifa mwenye umri mdogo lakini aliye makini na kazi yake.

Robinson Wangaso

Thursday, January 21, 2010

RAFIKI YANGU SIKUMFAHAMU ANA WIVU

Ni vigumu kufahamu tabia ya kila mmoja licha ya kuishi na mtu kwa muda mrefu hususani marafiki ambao tunao karibu.

Imewahi kunitokea kushauriwa vibaya na rafiki yangu kuacha kufanya mambo yenye mafanikio kwa kuwonawivu. Je wewe mkasa kama huu umewahi kukutokea?

Robinson Wangaso

MAPENZI / NGONO KAZINI !!! IWEPO SHERIA??

Sote tunatambua neno mapenzi linaashilia uhusiano mwema, japo Neno hilohilo kwa matumizi ya sasa na hali halisi limeweza kusababisha mtafaruku mkubwa kati ya mtu na mtu na hata kati ya wanandoa na kusababisha mahusiano ya watu hao kuwa mabaya, haya siyo mapenzi kama neno linavyojieleza kwani hakuna upendo hata kidogo, bali ni NGONO maofisini ambayo inatumoka kuzorotesha ufanisi wa kazi katika maeneo hayo.

Kwa leo tuangali mapenzi katika maeneo ya kazi hasa zaidi nazungumzia kati ya wakuu wa vitengo (Maofisa) ambao hupenda kuitwa mabosi jina baya kabisa na lisilofaa kwa Mtanzania mwenye nafasi ya kutumikia watu kujiita/ kuitwa ''BOSS''

Ni dhahili tunatambua mapenzi yanaweza kuvuruga ufanisi na utendaji kazi na hata kuondoa heshima dhidi ya wasaidizi, mapenzi katika ofisi nyingi yamesababisha watendaji wengi kuacha kazi kutokana na fitina na chuki dhidi ya wakubwa wao wa kazi. Pia wakubwa hao wanapolewa mapenzi huweza kuwapatia waangalizi wa ofisi yao (ps)madaraka yasioendana na sifa na uwezo wao.

hali kana hii inatupeleka wapi jamani?? nanyi semeni kamani haki kuona wazee wanatembea kimwili na watoto wadogo kwa kuwadanganyishia posho, malupulupu pamoja na nafasi ambazo siyo halali.

Kwa upande wa hao mabinti wadogo ambao wanalazimika kuwa na uhusiano wa kimapenzi ha hao wanaojiita MABOSS, ni kweli pamoja na kupewa upendeleo huo unadhani wako salama?? Ikitokea huyo mtu kahamishwa au kafariki kwa vile alikuwa anategemea kubebwa unadhaninutendaji kazi wake utakuwa vipi.

Kutokana na hali hiyo ya kubebwa kama JENEZA hivi ni kweli mfanyakazi huyo atakua salama na kazi yake kwa kutembea na Boss wake au kesho akipata mwingine anaempendeza machoni zaidi kuliko yeye mabo yatakuwa vipi??!! naombeni kwa hili nalo mnishauri.

mbaya zaidi hawa wanaojiita wafanyakazi wenye mahusiano ya kimapenzi wa Maboss wamekuwa wakitumia uhusiano huo kuwavuruga watumishi wenzao kwa wakubwa wao wa kazi na kutokana na wakubwa kulewa mapenzi huwachukia wafanyakazi hao bila kufanya uchunguzi wa kina.

Hawa wazee nao pia tuwape somo, wasiburuzwe na vibinti kisa wanamahusiano ya kimapenzi. wakumbuke kupewa nafasi yoyote ile ni kwa ajili ya kutumikia watu na siyo kujipatia vijitoto tena ni sawa na kuvibaka vitoto / vibinti hivyo ambavyo vinachafuliwa damu buila kujijua.

Baadhi ya mabinti hushiriki mapenzi na wazee hao kwa kuhofia kupoteza kazi au kupata upendeleo maalumu lakini wakati huo huo huwa na wapenzi wao vijana hata katika iofisi hizo ambao ni rika moja, hali hiyo inapojulikana maboss hao huwachukia wanaotembea na wasaidizi hao bila kujua siyo haki wala sawa kwa mzee kama huyo badala ya kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa wafanyakazi wake, anakuwa ndie mwanzilishi wa ugomvi, fitina kutoka na kuchangia binti mdogo kimapenzi na vijana.
Hapa naona umuhimu wa kutungwa kwa sheria ya mapenzi kazini kwani ukiongea na mabinti wengi wanaotembea na wakubwa wao wa kazi watasema walibakwa, walitishiwa kupoteza kazi, walipewa nafasi ya upendeleo na hata madaraka yasiyowasitahili hadi kushawishika.

Haya nanyi semeni.

Robinson Wangaso nahitaji ushauri na maoni yako.

USHIRIKINA KAZINI / MAOFISINI JAMANI

Ni kweli kwa siku za hivi karibuni, kumekuwepo na malalamiko mengi dhidhi ya vitendo vya kikatili na kinyama dhidi ya mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino)kutokana na vifO vyenye simanzi na masikitiko makubwa DHIDI YA BUNADAMU WENZETU.

Hali hii inatokana na wasomi tulionao kuwa na imani potofu juu ya ushirikina. Kama Mtu aliyesoma na kufuzu shahada/ stashahada, bado anaamini juu ya ushirikina. Mtu kama huyo kabla ya kuanza kazi anaanzia kwa mganga wa JADI ndipo aanze kazi. Wengine huenda mbali zaidi na hata kudriki kupeleka katika ofisui wanazofanyia kazi waganga ili wazindiki ofisi hizo wakidhani pasipo kufanya hivyo hawatakuwa salama. Je, hivi tunao wasomi au ni vyema turudi kwa Mababi na Mabibi zetu tuwaachie ofisi waziendeshe? kwani pamoja na kusomabado tunaamini bila ushirikina mambohayaendi.

Kama msomi anaamini ushirikina, anaenda kwa mganga kabla ya kuanza kazi au akazindike ofisi, Unadhani kati ya mganga na Mtu huyo anaejiita Msomi nani aachiwe ofisi. Nasisitiza hili kwa sababu huwezi kujua kesho mganga atamshauri nini huyo mwajiriwa mwenye kutegemea mganga na pasipo Ushirikina hajiiaminin kuwa yupo kazini.

Naombeni ushauri na mawazo yenu juu ya suala hili. Hawa wasomi Tegemezi, hawatufai kamwe kuendelea kuwa nao katika ofisi yoyote ile ni kuwa na mtu hatari kwa maendeleo ya taifa. Ni msimamo na Mtazamo wangu tu, Nawe toa wako.

Robinson Wangaso