Wednesday, September 15, 2010

BUTIAMA WAMPONGEZA JK

Na Robinson Wangaso, Musoma - MARA 0784301526, 0765632944

Wananchi wa kata za Butiama ,Masaba, Muryaza na Butuguri wilayani Musoma vijijini mkoani Mara wamefanya maandamano ya kumpongeza rais Jakaya Kikwete kwa kuiteua Butiama kuwa wilaya mpya.

Sherehe hizo zimefanyika jana kijijini Butiama katika ukumbi wa Joseph Kizurira Nyerere ambao ulishatumika kuikutanisha Halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM chini ya uongozi wa mwenyekiti wa chama hicho taifa Jakaya Kikwete na kutoa pendekezo la jina la Butiama kupewa wilaya mpya itakayoundwa kutoka wilaya ya Musoma vijijini.

Maandamano hayo ambayo yameanzia katika vijiji mbalimbali vya kata hizo yamepokelewa mkuu wa wilaya ya Musoma ambae aliwakilishwa na Afisa Tarafa ya Makongoro Lucy Makenge na viongozi mbalimbali waandamizi kutoka halmashauri ya wilaya.

Bi Lucy Aliwaasa wakazi wa Butiama kuwa tayari kushirikiana na kuijenga wilaya hiyo mpya ili kumuenzi Baba wa Taifa Mwali Julius Kambarage Nyerere kwa mambo mazuri aliyoyafanya katika kuongoza nchi na amewathibitishia wananchi hao kuwa saerikali ya jamuhuri ya Muungano itatimiza azma yake ya kuanzishwa na kuiendeleza wilaya mpya ya Butiama.

" Kwa niaba ya familia ya mwalimu Nyerere, anatoa shukrani kwa Rais Kikwete kwa kuona umuhimu wa kuanzisha wilaya mpya yenye jina la Butiama, kijiji alichozaliwa Baba wa Taifa" alisema Lucy, Afisa tarafa.

Akiongea kwa niaba ya wazee wa kijiji cha Butiama, Mzee Jackton Nyerere alisema " Nyerere Burito baba yake na mwalimu Nyerere kabla ya kifo chake aliwahi kutabiri kuwa Butiama itakuwa na wageni wa kila aina, kuanzishwa kwa wilaya hii ni kukamikilika kw utabiri wa Chiefu huyo wa kabila la wazanaki" alisema mzee Jackton Nyerere.

Nae Mwalimu Jack Nyamwaga alisema kikao cha Halmashauri kuu ya taifa kufanyika Butiama kilikuwa na jambo ambapo Tanzania imeweza kuazimia mabo mengi ikiwemo azimio la Arusha, siasa na kilio, Azimio la Musoma anazimio la Mwisho kwa mjibu wa mwlimu huyo ni kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Butiama.

Hafla hizo pia zimeandaman na ngoma, kwaya, michezo mbalimbali ziikiwemo ya asili kutoka kabila la Wazanaki, Waikizu ambapo maelfu ya wananchi kutoka kata jirani na Butiama wamehudhuria.

kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Butiama Zakaria Wambura alisema Ris Kikwete amemuenzi baba wa taifa kwa vitendo kwa ambapo wilaya hiyo mpya itakuwa chachu katika kuinua hali za maisha ya wananchi wa kata hiyo na kata jirani

Wakati huo huo mmoja wa wanafamilai ya mwalimu Veronica Jackton Nyerere ametangania nia ya kuwania nafasi ya ubunge vitri maalumu mkoani Mara kupitia ambae amewataka wananchi hao kutoshangilia wilaya mpya na kuwapisha wageni, bali wafanye kazi kwa bidii.

"Wanabutiama tuwe wabunifu ili wilaya iwe wilaya mfano ya kumuenzi baba wa taifa na tukubali kubadilika na kuwasomesha watoto ili kuendana na soko la ajira" alisema Veronica Nyerere mbele ya umati huo.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment