Wednesday, September 15, 2010

UCHAGUZI SWEDEN

Na Robinson Wangaso, Sweden +46722071257.

Jumapili ijayo ni siku muhimu kwa Wananachi wa Sweden ikiwa ni siku ya uchaguzi wa kuwapata viongozi wao wa kisiasa katika ngazi ya majimbo, mkoa na wawakilishi katika Bunge sawa na ngazi ya kitaifa.

lakini kwa Waswidi zoezi la kupiga kura limeanza wiki moja kabla kwa wale anaodhani siku hiyo hawatakua na nafasi kwenda kupiga kura wanafika kwa wakati wao wanaopenda katika vituo vilivyopo wanapiga kuza zao na kuondoka.

Kilichonistajabisha zaidi ni pale nilipotembelea kituo kimojawapo cha kupiga kura katikati ya jiji la Stockholm ambao ndiyo mji mkuu wa nchi hii na kujionea jinsi kura hizo zinavyopigwa katika hali ya uwazi.

Japo kura ni siri lakini wakati mtu anapopiga kura yake katika eneo la kupigia kura unaweza kusogea karibu bila wasiwasi kama ilivyozoeleka nyumbani nchini Tanzania bila shaka nawe utapiga kura yako na kuondoka.

Zaidi ya hapo katika chumba cha kupigia kura nilikuta watu wawili ambao ndio wasimamizi wa upigaji kura hakuna mawakala wa vyama vya siasa na watu wanawaamini na kupiga kura zao bila kuhofia kuwa kura zitaibiwa jambo ambalo lilinishabgaza kuona hivyo tume ya uchaguzi kusimamia upigaji kura kwa kuaminiwa na wananchi pamoja na wanaogombea kupitia vyama mbalimbali vya siasa.

Kuhusu kampeni kama tunavyojua juma la mwisho huwa ni vurugu mechi lakini ukiwa nchini Sweden hutajua kua ni wiki ya Uchaguzi kama hujaambia na mtu kwani kampeni hazifanyiki katika mikutano ya hadhara bali ni kupitia vyombo vya habari na kuwasambazia majumbani vipeperushi wananchi kupitia masanduku yao ya Barua (Posta)vinavyoelezea sera za vyama vyao.

Pia katika baadhi ya niji na majiji unakuta wafuasi wachache wa vyama fulani wakigawa machapisho hayo ya sera kwa watu wanaopenda kujua juu ya chama hicho lakini kazi hiyo inafanyika katika hali ya utulivu na hakuna vurugu wala kulazimishwa kuchukua kipeperushi bali kwa kuombwa kwa lungha ya unyenyekevu kuchukua vipeperushi.

Mfumo wa uchaguzi ni kuchagua Chama na siyo mtu, kila chama kinakua na orodha ya wagombea ambao watateuliwa kuingia bungeni Mara baada ya uchaguzi ikiwa kitashinda lakini watakaoteuliwa inategemeana na asilimia ya ushindi au kura chama kilichopata.

Lakini pia mpiga kura kabla ya kupiga ataangalia orodha ya wagombea wa chama anachokipenda na ikia ataona mtu anaempenda amewekwa katika orodha nafasi ya mwisho kwa umuhimu anaweza kuzungushia jina lake kuonyesha kua mtu huyo anapenda apewe nafasi kutokana na kua anapenda aiingie Bungeni.


Pamoja na wagombea kupewa nafasi za kipaumbele na vyama vyao pia wananchi au wapiga kura wanayo fursa ya kubadilisha orodha kwa kumpigia mtu furani aliyopewa nafasi ya mwisho na kupewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwawakilisha katika bunge ikia ni namna ya kuthamini na kuheshimu wanachokipenda wapiga kura.

Zaidi ya vyama Saba zinashiriki katika uchaguzi utakaofanyika Wiki hii hapa nchini Sweden huku hakuna kelele wala vurugu zozote zinazoashiria kuwepo na uchaguzi watu wakiendelea na shughuli zao kamakawaida.

Wanaoruhusiwa kupiga kura ni raia wa Swedena na wageni ambao siyo raia lakini wenye vibali (VISA) za zaidi ya miaka mitatu kuishi nchini humo nao wanayo haki ya kupiga kura hata kama siyo raia wa nchi hiyo.

Sweden ni nchi inayofuata mfumo wa utawala wa Kifalme lakini ikiwa na vyama vingi vya siasa na kiongozi mkuu na msimamizi shughuli za serikali ni waziri mkuu ambae huchaguliwa kwa kupigia kura kila baada ya miaka minne.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment