Thursday, January 21, 2010

MAPENZI / NGONO KAZINI !!! IWEPO SHERIA??

Sote tunatambua neno mapenzi linaashilia uhusiano mwema, japo Neno hilohilo kwa matumizi ya sasa na hali halisi limeweza kusababisha mtafaruku mkubwa kati ya mtu na mtu na hata kati ya wanandoa na kusababisha mahusiano ya watu hao kuwa mabaya, haya siyo mapenzi kama neno linavyojieleza kwani hakuna upendo hata kidogo, bali ni NGONO maofisini ambayo inatumoka kuzorotesha ufanisi wa kazi katika maeneo hayo.

Kwa leo tuangali mapenzi katika maeneo ya kazi hasa zaidi nazungumzia kati ya wakuu wa vitengo (Maofisa) ambao hupenda kuitwa mabosi jina baya kabisa na lisilofaa kwa Mtanzania mwenye nafasi ya kutumikia watu kujiita/ kuitwa ''BOSS''

Ni dhahili tunatambua mapenzi yanaweza kuvuruga ufanisi na utendaji kazi na hata kuondoa heshima dhidi ya wasaidizi, mapenzi katika ofisi nyingi yamesababisha watendaji wengi kuacha kazi kutokana na fitina na chuki dhidi ya wakubwa wao wa kazi. Pia wakubwa hao wanapolewa mapenzi huweza kuwapatia waangalizi wa ofisi yao (ps)madaraka yasioendana na sifa na uwezo wao.

hali kana hii inatupeleka wapi jamani?? nanyi semeni kamani haki kuona wazee wanatembea kimwili na watoto wadogo kwa kuwadanganyishia posho, malupulupu pamoja na nafasi ambazo siyo halali.

Kwa upande wa hao mabinti wadogo ambao wanalazimika kuwa na uhusiano wa kimapenzi ha hao wanaojiita MABOSS, ni kweli pamoja na kupewa upendeleo huo unadhani wako salama?? Ikitokea huyo mtu kahamishwa au kafariki kwa vile alikuwa anategemea kubebwa unadhaninutendaji kazi wake utakuwa vipi.

Kutokana na hali hiyo ya kubebwa kama JENEZA hivi ni kweli mfanyakazi huyo atakua salama na kazi yake kwa kutembea na Boss wake au kesho akipata mwingine anaempendeza machoni zaidi kuliko yeye mabo yatakuwa vipi??!! naombeni kwa hili nalo mnishauri.

mbaya zaidi hawa wanaojiita wafanyakazi wenye mahusiano ya kimapenzi wa Maboss wamekuwa wakitumia uhusiano huo kuwavuruga watumishi wenzao kwa wakubwa wao wa kazi na kutokana na wakubwa kulewa mapenzi huwachukia wafanyakazi hao bila kufanya uchunguzi wa kina.

Hawa wazee nao pia tuwape somo, wasiburuzwe na vibinti kisa wanamahusiano ya kimapenzi. wakumbuke kupewa nafasi yoyote ile ni kwa ajili ya kutumikia watu na siyo kujipatia vijitoto tena ni sawa na kuvibaka vitoto / vibinti hivyo ambavyo vinachafuliwa damu buila kujijua.

Baadhi ya mabinti hushiriki mapenzi na wazee hao kwa kuhofia kupoteza kazi au kupata upendeleo maalumu lakini wakati huo huo huwa na wapenzi wao vijana hata katika iofisi hizo ambao ni rika moja, hali hiyo inapojulikana maboss hao huwachukia wanaotembea na wasaidizi hao bila kujua siyo haki wala sawa kwa mzee kama huyo badala ya kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa wafanyakazi wake, anakuwa ndie mwanzilishi wa ugomvi, fitina kutoka na kuchangia binti mdogo kimapenzi na vijana.
Hapa naona umuhimu wa kutungwa kwa sheria ya mapenzi kazini kwani ukiongea na mabinti wengi wanaotembea na wakubwa wao wa kazi watasema walibakwa, walitishiwa kupoteza kazi, walipewa nafasi ya upendeleo na hata madaraka yasiyowasitahili hadi kushawishika.

Haya nanyi semeni.

Robinson Wangaso nahitaji ushauri na maoni yako.

No comments:

Post a Comment