Tuesday, January 26, 2010

CHANGAMOTO KAZINI ZINATUKOMAZA, TUSIHOFU.

Kumekuwepo na badhi ya watumishi kupenda kuwasingizia watumishi wenzao makazini kwa mambo yasiyokuwa na msingi kwa malengo wa kuwakosanisha watu, marafiki, wafanyakazi ama mtu na mkuu wake wa kazi.

Kwa wale wanaowafanya vitendo hivyo wakumbuke kuwa nao ipo siku nao watafanyiwa vivyo hivyo japo katika maeneo tofauti ya kazi kutokana na usemi usemao, kila mtu atapimiwa kipimo kilekile alichopimia wenzake, na pia malipo ya mambo yote ya duniani ni hapa duniani. Katika mandiko matakatifu yanasema usihukumu ili nawe usije ukahukumiwa.

Inatia faraja kwa wanaofanyiwa hivyo wasife moyo kwani zamu yao imekwisha wangojewe thawabu kwa mambo hayo na wasikate tamaa bali wawe na moyo wa ujasiri na uvumilivu katika kuzikabiri changamoto hizo. Kwa hili namkumbuka hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere ambae aliwahi kusema ' Mtu Madhubuti mwenye moyo thabiti, haogopi matatizo bali hukomazwa nayo' mwisho wa kumnukuu.

Robinson Wangaso- Musoma MARA

No comments:

Post a Comment