Wednesday, November 4, 2009

NI JUKUMU LA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA UFISADI- ASKOFU

Askofu Michael musongazila (wa pili Kulia)na wa pili Kushoto ni Padre pius msereti mara baada ya Upadirisho- Nyamuswa Ikizu

Jaji Joseph Sinde Warioba akimpongeza Padre mpya Pius Msereti Mara baada ya kupadirishwa, Picha na Robinson Wangaso - Mara



Kanisa katoliki limesema ni jukumu la viongozi wa kanisa hilo kukemea vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya viongozi hapa nchini ukiwemo ufisadi ili kuweza kuving'oa, kuvibomoa na kuviangamiza.

Kauli hiyo hiyo ilitolewa Julai 9 mwaka huu 2009 na askofu wa kanisa Katholiki jimbo la Musoma mhashamu Michael Msonganzila katika sherehe za upadirisho wa padre mpya Pius Msereti uliyofanyika katika parokia ya Nyamuswa - Ikizu wilayani bunda mkoani Mara.

Askofu Msonganzila alisema kanisa haliandai wagombea wa nafasi mbalimbali za siasa kama ilivyodaiwa na baadhi ya wanasiasa bali linaandaa waamini wake kushiriki katika uchaguzi ujao kwa umakini na kujiepusha na vitendo vya rushwa na kuchagua viongozi wasiyo faa.

"Ni wajibu wa viongozi wa kanisa Kung'oa, kubomoa na kuangamiza kwa kukemea maovu kwa neno la mungu na siyo kukaa kimya vikiwemo vitendo vya ufisadi" alisema Msonganzila.

Alisisitiza kuwa kamwe kanisa halitakaa kimya huku maovu yakiendelea katika jamii na wanachi wakiwa wanataabika kwani seriakli ya tanzania haina dini na wala serikali hiyo siyo ya dini yoyote.

Katika hatua nyingine alisema mapigano yanayoendelea katika wilaya ya Tarime na Rorya yanatokana na ugumu wa mioyo ya wanachi hao na viongozi wa dini inapaswa wayakemee pasipo kuogopa upande wowote ule.

Alisema ni hali ya kusikitisha kuona watu wanauwana bila hatia huku hali hiyom ikiendelea kufumbiwa macho.

Upadrisho huo wa padre Pius Msereti wa kwanza katika Parokia ya Nyamuswa na ni padre wa kwanza kutoka katika kabila la WAIKIZU na umehudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo mama Maria Nyerere, Waziri mkuu wa zamani Jaji Joseph Sinde Warioba ambae pia walitoa zawadi kwa niaba ya rais mstaafu wa awamu wa tatu Benjamin William Mkapa na viongozi mbalimbali waandamizi waserikali na vyama mbalimbali vya siasa.Kwa hili pia namshukru shakila omary kwa ushauri wake na mchango wa mawazo aliyotoa na Annastazia kutoka SAUT.



href="http://1.bp.blogspot.com/_-mB36LBfMg4/SvFQTyy6xxI/AAAAAAAAABU/EgcstdgzgO
/s1600-h/DSC01302.JPG">



,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment