Wednesday, November 4, 2009

Waikizu ni wakulima/ wafugaji na wawindaji - Mara

jaji Warioba akitoa zawadi kwa niaba ya rais Benjamini William Mkapa - Nyamuswa.

Wanawito wasichana wa parokia ya Nyamuswa wakiserebuka katika kanisa wakati wa misa ya upandirisho wa Pius Msereti.

Wakristo wa parokia ya Nyamuswa Ikizu wakitoa zawadi ya ng'ombe kwa padre pius Msereti kama ishara ya kabila hilo ambalo ni wakulima, wafugaji na wawindaji mashuhuri hapa nchini.



Kabila la WAIKIZU wanaoishi mkoani Mara ni maarufu kwa kulima mzao la Mihogo kwa ajili ya chakula, na wafugaji wa mbuzi, kondoo na Ng'ombe kuhu kabila hilo likiwa maarufu kwa UWINDAJI wa wanyama pori.

Kabila hilo ambalo desturi zake ni za Kijamaa ni kabila maarufu mkoani Hapa ambalo hujulikana kwa kutokuwa na majivuno, bali watu wake hufanya kazi kwa ushirikiano hasa wakati wa msimu wa kilimo ambapo watu hulima mara nyingi kwa ushirikiano (LISAGA)kwa kabila hilo.

Pamoja na kuwa wawindaji, pia wamepata padre wa kwanza katika Parokia ya Ikizu - Nyamuswa (Padre Pius Msereti)

No comments:

Post a Comment