Wednesday, November 4, 2009

Waikizu wapata Padre wa Kwanza - Mara


Mama Maria Nyerere akipongeza padre pius Msereti mara baada ya kupokea daraja la upadre katika parokia ya Nyamuswa- Ikizu











Mapadre wa jimbo la Musoma wa kushoto (Mzungu) kutoka kwa pius Msereti ni paroko wa parokia ya kiabakari padre Voichek Adamu





Padre mpya Pius Msereti (kushoto) akisaini cheti cha upadrisho mbele ya Mwashamu askofu Michael(kulia) Msongazila wa jimbo Katholiki Musoma wa katikati Padre Chegere katibu wa askofu.



Tarehe 9 Julai ya mwaka 2009 ni siku muhimu na ya kumbukumbu muhimu kwa Kabila la waikizu kutokana na tukio la kihistoria ambayo haitabadilishwa na mtu yeyeote kutokana na umuhimun wake. Kwa mara ya kwanza siku hiyo kabila la Waikizu ambao wanaishi mkoani Mara, licha ya kuwa na viongozi mashuhuri wa kisiasa Nchini wasliowahi kushika nyadhifa mbalimbali akiwemo Waziri mkuu wa zamani na makamu wa kwanza wa rais wa Serikali ya awamu ya pili ambae pia aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikli, Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Kilimo chakula na Ushirika wa sasa Stephen Masatu Wasira, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi nchini marehemu Peter Nyamuhokya na viongozi wengineo, wamepata Padre Pius Msereti kwa mara ya kwanza.

Msereti anaonekana kuwa kiongozi wa kihistoria katika kabila hilo kutokana na Mambo ya imani kuwa na umuhimu wa pekee katika jamii ambapo sherehe ya upadirisho huo ilihudhuriwa na watu wenge huku rais mstaafu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Benjamin willia Mkapa akiwakilishwa na Jaji warioba, Mama MAria Nyerere na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali za kitaifa wakishuhudia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment